Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),Profesa Dos Santos Silayo (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan (kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano kati ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akishuhudia tukio hilo katika mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan (kulia) mara baada ya kusaini mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akishuhudia tukio hilo kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Santos Silayo (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas, Hamisi Ramadhan (kulia) wakionesha hati ya makubaliano mara baada ya utiaji saini mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya Mihan Gas wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa Umma ili kupunguza matumizi ya mkaa huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akishuhudia tukio hilo kwenye mkutano uliofanyika jana jijini Dodoma.

Na Mwandishi wetu.

Serikali imesaini mkataba na Kampuni ya Gesi ya Mihan Gas wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa umma.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni juhudi za Serikali za kutaka kupunguza matumizi ya mkaa pamoja na kuni kwa lengo la kutaka kuhifadhi misitu ambayo imekuwa ikitumika kama nishati.

Mkataba huo ulisainiwa jana Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),Profesa Dos Santos Silayo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mihan Gas, Hamisi Ramadhan na huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Mej. Gen. Gaudence Milanzi akishuhudia tukio hilo.

Mbali na kusaini mkataba huo, TFS na Kampuni ya Mihan Gas zilizindua kampeni ya kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vya vyake kwa Watumishi wa Umma.

Awali, Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Milanzi aliwahimiza watumishi kuchangamkia fursa hiyo ya kukopa mitungi na vifaa hivyo kwani itasaidia katika kuokoa misitu.

“Hili ni tukio kubwa hasa kwa wale ambao ni watunzaji wa mazingira katika kuwezesha jamii kuanza kutumia nishati mbadala.’’ Alisema

Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu zaTanzania (TFS),Profesa Dos Santos Silayo,alisema upatikanaji wa huduma hiyo ni jitihada za kuhakikisha matumizi ya mkaa yanapungua

Aliongeza kuwa nishati mbadala ndo njia pekee itakayosaidia jamii kuachana na matumizi ya mkaa na kuni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,Hamisi Ramadhani aliishukuru Serikali kwa kuikubalia kampuni hiyo kusambaza gesi kwa watumishi.

Akizungumzia namna watumishi watakavyonufaika na mpango huo, Mkurugenzi Mtendaji , Ramadhani alisema kampuni imetenga fungu ambalo litarahisisha ukopeshaji wa vifaa hivyo na kila Mtumishi atapewa nafasi ya kuweza kulipia mwezi mmoja mara baada ya kuanza kuitumia gesi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: