Mkuu wa Mawasiliano kutoka Umoja wa Mataifa Hoyce Temu akiongea na waandishi wa habari na kufafanua baadhi ya mambo baada ya kikao cha mafunzo kwa vijana 20 wenye ulemavu uliofanyika mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Seed Trust Magreth Nkanga, ambaye pia ni mbunge mstaafu aliyekuwa akiwakilisha kundi la walemavu akishukuru un kwa kutoa machapisho maalum takribani 1000 yaliyoandikwa kwa lugha ya alama, yakihusu mkakati ya elimu ya malengo endelevu ya dunia
 Kijana mwenye ulemavu wa macho Godbless Muro, mwanafunzi wa shahada ya sayansi ya siasa na utawala,chuo kikuu Dodoma akisoma moja ya chapisho iliyoandikwa kwa maandishi ya nundunundu yenye ujumbe wa maendeleo endelevu ya kidunia.
 Vijana mbalimbali wenye ulemavu sambamba na waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini wakati wakikao cha utoaji elimu ya malengo endelevu a dunia kilichofanyika mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Seed Trust kushoto Steven Mashishanga akimkabidhi Katibu Tawala Msaidizi, mkoa wa Morogoro Ernest Mkongo moja ya chapisho maalumu kwa watu wenye ulemavu la mpango wa elimu ya maeneleo ya dunia, (katikati) Mkuu wa Mawasiliano kutoka Umoja wa Mataifa Hoyce T emu.
---
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kwa kushirikiana na Shirika la Seed Trust wameanzisha timu ya Vijana 20 wenye ulemavu wa aina mbalimbali kutoka Vyuo Sita Vya Elimu ya Juu nchini kwaajili ya kufanya ushawishi na utetezi kwa wanafunzi wenye ulemavu ili kuwajengea uwezo wa kusaidia maendeleo endelevu ya kidunia.

Mafunzo hayo ambayo yameshirikisha wanavyuo walemavu kutoka vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini yanatoa nafasi ya kundi la watu wenye ulemavu kuweza kushirikishwa katika utekelezaji wa mwaka wa pili wa elimu ya malengo endelevu ya dunia yanayosema hakuna binadamu yeyote atakaye achwa nyuma

Katika mafunzo hayo Umoja Wa Mataifa umetoa machapisho maalum takribani 1,000 yaliyoandikwa kwa lugha ya alama yatakayowezesha watu wenye ulemavu wa macho kusoma na kuelewa mipango ya maendeleo endelevu ya kidunia

Katika kutekeleza malengo hayo vijana hao watafundishwa pamoja na kuzunguka kuhamaasisha malengo hayo kwa walemavu wengine katika vipaumbele mbali mbali ikiwemo elimu na afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: