Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (katikati) akizunguza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka kumo ya kuanzishwa kwa huduma ya M-Pesa nchini Tanzania leo katika ukumbi wa Makao makuu ya Vodacom hapa nchini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mwendelezo ya Biashara ya M-Pesa, Polycarp Ndekana na kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kulia) akitoa zawadi kwa mwandishi wa EATV, Njonanje Samwel (kushoto) wa habari ambaye alikuwepo wakati wa uzinduzi wa huduma ya M-Pesa 2008
Mkuu wa Kitengo cha Mwendelezo ya Biashara ya M-Pesa, Polycarp Ndekana akizungumzia namna walivyojiimarisha kwenye huduma ya M-Pesa hapa nchini pamoja na nje ya nchi wakati wa maadhimisho ya miaka Kumi ya kuanzishwa kwa huduma ya M-Pesa hapa nchini kupitia mtandao wa Vodacom.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia akitoa ufafanuzi kuhusu huduma za Mpesa zinazotolewa na Mtandao wa Vodacom hapa nchini.
---
Vodacom Tanzania PLC leo imetimiza miaka kumi tangu kuzinduliwa kwa huduma ya M-Pesa. Kwa miaka hiyo kumi, Vodacom M-Pesa imejikita kwenye huduma mbali mbali kama kulipia huduma na bidhaa, huduma za kibenki, kuweka na kukopa pesa, kutuma pesa nje ya nchi na zingine nyingi. Huduma hizo zote zinatokana kwa njia rahisi sana ya huduma ya pesa kwa njia ya mtandao ambayo ilikuwepo tangu mwanzoni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Vodacom Tanzania Ian Ferrao alisema, M-Pesa imeweza ajira za moja kwa moja na ambao sio za moja kwa moja zaidi ya 200,000- wengi wao wakiwa ndio wanaanza ujasiriamali – na kufanya zaidi ya Tzs 617 bilioni kulipwa kama kasmine kwa mawakala kila mahali Tanzania.

Zaidi ya Tzs 120 bilioni zimetolewa kama mikopo tangu kuzinduliwa kwa M-Pawa (huduma ya kuweka na kukopa) mwaka 2014 na hivyo kufanya wajasiriamali kuanzisha biashara mpya na hivyo kubadilisha hali ya maisha yao ya kila siku. Mpaka sasa zaidi ya Tzs 99 bilioni zimetolewa kama faida kwa watumiaji wa M-Pesa milioni 8 na zaidi ya Tzs 355 bilioni zimewekezwa kwenye benki mbali mbali hapa Tanzania. Hii inaamanisha kuwa M-Pesa, pesa yako inaendelea kutengeneza faida kupitia kwenye akaunti yako.

Mafanikio ya M-Pesa kwa miaka kumi iliyopita inamaanisha mwanzo mpya wa malipo kwa njia ya kidijitali hapa Tanzania. M-Pesa imenguza na kubadilisha maisha ya mamilioni ya Watanzania pekee. Miaka kumi iliyopita, M-Pesa ilimaanisha kutuma na kupokea pesa kutoka kwa mteja mmoja kwenda kwa mwingine.

Ian alipongeza juhudi za Vodacom kuboresha na kukuza huduma ya fedha kwa simu za mkononi hapa Tanzania na kuchangia kukuza uchumi wa Tanzania kwa kutengeneza ajira, kukuza biashara na sana sana wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na kukuza uchumi wa nchi. Leo zaidi ya 35% uchumi wa nchi – GDP unachangiwa kwa kupitia M-Pesa huku kila mwezi ziaidi ya miamala yenye thamani ya 1.2 trilioni ikifanyika.

Kusherekea miaka kumi ya mafanikio ya Vodacom M-Pesa kuna kuja baada ya kuzawadiwa zawadi ya GSMA Mobile certification kwa usalama na utaalam uliotukuka na kuifanya Vodacom M-Pesa moja na bidhaa za kampuni za simu za mkononi kupata cheti cha kimataifa.

Ian Ferrao aliongeza kuwa maadhimisho ya kutimiza miaka kumi yatafanyika mikoa mbali mbali hapa Tanzania ikiwa ni kwa kampuni kuonyesha shukrani kwa wafanyakazi, mawakala wa M-Pesa, wafanyabiashara ambao kwa pamoja wameweza kuchangia safari hii ya mafanikio.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: