Pichani ni gari namba STK 5923 aina Toyota Landcruiser mali ya Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji iliyokuwa ikiendeshwa na Priscus Peter(23) mkazi wa Dar es Salaam kugongana na scania namba T 620AQV/ T 407DBY na kupelekea vifo na majeruhi. 
WATENDAJI watatu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wakiwamo Wakurugenzi wawili na Meneja mmoja wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kupata ajali ya kugongana uso kwa uso na Scania katika Kijiji cha Msoga Chalinze mkoani Pwani.

Akizungumza na kwa njia ya simu leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Jonathan Warioba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusababisha vifo hivyo ambapo amesema Zacharia Kingu na Martin Masalu ambaye ni Meneja wa Utafiti walifariki papo hapo wakati Said Amir alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali kwa matibabu.

Amefafanua ajali hiyo imehusisha magari mawili ambayo ni gari namba STK 923 aina Toyota Landcruiser mali ya Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji iliyokuwa ikiendeshwa na Priscus Peter (23) mkazi wa Dar es Salaam kugongana na scania namba T 620AQV/ T 407DBY.

"Mei 21 mwaka huu saa 15:30 maeneo ya Msoga-Chalinze katika barabara ya Msoga/Msolwa Wilaya ya kipolisi Chalinze Mkoa wa Pwani, gari hizo ziligongana na kusababisha vifo na majeruhi,"amefafanua Kamanda Warioba.

Ameongeza majeruhi katika ajali hiyo ni Godfrey Kilolo (45) na dereva Priscus Peter ambao walipelekwa Hospitali ya Msoga kwa matibabu na tayari wameruhusiwa na miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani.

Eneo la ajali hiyo kwa mujibu wa taarifa limekaguliwa na na ASP. Solla-Occid (W) akisaidiwa na INSP. MS Mkojera - DTO (W) Chkojera pamoja na F7704 PC Hamza ambaye ndiye mpelelezi wa tukio hilo.Hata hivyo juhudi za zinafanyika kumpata dereva wa Scania kwa mahojiano zaidi kwani alikimbia baada ya ajali kutokea.

Uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari namba STK 5923 T ambaye alihama kutoka upande wake na kwenda kugongana na Scania hiyo.
===
CHAL/TR/AR/11/2018 ILANI YA KWANZA: KOSA AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA KUSABABISHA VIFO, MAJERUHI NA UHALIBIFU WA MAGARI HAYO:

Mnamo tarehe 21/05/2018 majira ya saa 15:30hrs huko maeneo ya kijiji cha Msoga- Chalinze, barabara ya Msoga/Msolwa wilaya ya kipolisi Chalinze Mkoa wa Pwani, gari no STK. 5923 aina TOYOTA LANDCRUISER mali ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ikiendeshwa na dereva aitwae PRISCUS s/o PETER, 23yrs, Mchaga, mkristo, mkazi wa DSM, aligongana na gari no. T. 620AQV/ T. 407DBY aina ya SCANIA ikiendeshwa na dereva asiyefahamika jina, jinsia ya kiume kwani alitoroka mara tu baada ya ajali na kusababisha vifo vya watu wawili ambao ni MARTIN s/o LAURENCE@ MASALU, 39yrs, msukuma, meneja wa kanda, mkazi wa DSM na ZACHARIA s/o NALIGIA@ KINGU, 49yrs, Mnyiramba, mkazi wa DSM na majeruhi.kwa GODFREY s/o KILOLO, 45yrs, Mhehe, mkristo,mkazi wa DSM na PRISCUS s/o PETER, 23, dereva, Mchaga, mkristo, mkazi wa DSM.

Miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya Tumbi kusubili uchunguzi wa daktari. Majeruhi wamepelekwa hospitali ya Msoga kwa matibabu zaidi. Juhudi zinafanyika kuweza kumpata dereva wa lorry kwa mahojiano zaidi. Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari no STK 5923 T/LANDCRUISER kuhama kutoka upande wake na kwenda kugongana na gari no. T. 620 AQV/ T. 407DBY SCANIA.

Eneo la tukio limekaguliwa na ASP. W.M SOLLA- OCCID (W) Chalinze akisaidiwa na INSP. MS MKOJERA- DTO (W) Chalinze pamoja na F7704 PC HAMZA ambaye ndiye mpelelezi wa shauri hili. FCR/maendeleo inafuata Toka polisi traffic (w) Chalinze.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: