Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa kuhitimisha fainali za shindano la Shika Ndinga linaloendeshwa na kituo cha Radio cha Efm na Tv, Kwa kuwapongeza kuwa kituo cha kwanza kuwakumbuka wasikilizaji wake kwa kuwawezesha kuwa Wajasiliamali.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akikabidhi zawadi ya gari kwa Mshindi wa shindano la Shika Ndinga kwa Wanaume ambaye ametokea mkoa wa Tanga.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe  akikabidhi Zawadi ya gari kwa Mshindi wa Shika Ndinga kwa Wanawake ambaye anatokea Mkoa wa  Mwanza
 Meneja wa Kituo Cha Radiio cha EFM na Tv E, Dennisi Busulwa (Sebo) akizungumza na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofika kushuhudia fainali za shindano la Shika Ndinga katika Viwanja vya Tanganyika Parker's Dar es Salaam.
 Watangazaji wa Kipindi cha Ubaoni kutoka Radio ya Efm, Mpoki na Dokii wakishangilia na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofika katika fainali za shindano hilo katika Viwanja vya Tanganyika Parker's.
 Washiriki wa Shindano la Shika Ndinga kwa Wanawake  wakiwa katika harakati za kujaza Vikombe katika hatua ya kwanza ya shindano hilo.

Majaji wa Shindano la Shika Ndinga wakiwa wamesimama tayari kwa ajili ya kutizama mchezo utakavyoendelea uwanjani.
 Washiriki wa Kiume wakiwa katika hatua ya Mwisho ya kushika ndinga hili waweze kutwaa gari kwa atakayebaki mpaka mwisho
 Mmoja ya Washiriki kutoka mkoa wa Mtwara aliyotolewa katika hatua ya kwanza akitoa machozi mara baada ya kuenguliwa kwenye shindano.
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakifatilia shindano la Shika ndinga.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: