ABIRIA wanaosafiri kwenda katika mikoa ya Kusini hususani Lindi na Mtwara, wameulalamikia Uongozi wa Manispaa ya Temeke kwa hatua zake za kuwahamisha huduma za usafiri kwa mabasi hayo kutoka kituo Namba 21 kwenda Namba 48 vilivyopo eneo la Mbagala Jijini Dar es Salaam, hatua inayowafanya wapate usumbufu .

Wakizungumza na waandishi wa habari katika maeneo hayo, abiria hao wamesema kitendo hicho pamoja na mambo mengine, kimekuwa kisiwasababishia baadhi yao kupoteza mizigo na wakati mwingine kulazimika kutumia fedha za ziada kwa ajili ya kukodi piki piki na hata mikokoteni kuyafata mabasi hayo katika kituo Namba 48, ambacho kipo mbali na eneo la Barabara Kuu mahali walipokuwa wakipandia hapo awali.

Abiria hao akiwemo Mustafa Salehe, amesema kubadilishwa kwa utaratibu wa mabasi hayo kutoka kituo namba 21 kwenda kituo namba 48, kumesababisha changamoto kubwa kwa mamia ya abiria hasa wale wanaotumia kiruo hicho cha Mbagala, eneo ambalo ndilo linalotumika kama kituo kikuu cha daladala kutoka maeneo mbalimbali ya mji.

“Zamani ulikuwa ukishuka hapa kutoka mahali popote ndani ya mji huu, moja kwa moja unaingia katika basi kuendelea na safari yao, lakini kwa sasa inashangaza kuona huduma hiyo imeondolewa tena kwa baadhi ya mabasi, suala linaloleta wasiwasi kuwa pengine kuna mgogoro unaoendelea baina ya uongozi na wamiliki wa mabasi hayo” amesema Salehe.

Naye abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mwanakopa Hassan, mbali na kudai kushangazwa na hatua hiyo, amesema hali ya usafiri katika kituo hivyo imekuwa ya kutoeleweka kutokana na mkanganyiko unaojitokeza mara kwa mara mahali hapo.

“Hapo zamani tulikuwa tunapandia kituo hiki kikubwa cha daladala cha Rangi tatu ( kituo namba 21), baadae tukahamishwa tena kwenda huko mitaani (Namba 48), lakini kabla hatujakaa vizuri huduma zikarudishwa tena eneo la mara ya kwanza, na sasa wamezipeleka tena huko huko mitaani, jambo ambalo sisi kama abiria linatuchanganya ikizingatiwa siyo kila mtu mwenyeji wa mji huu” amesema Mwanakopa
Hata hivyo kwa mujibu wa abiria hao, huduma hizo za usafiri zimehamishwa kituo hicho kwa kampuni mbili za mabasi ambaazo ni Ngombale pamoja na Mashallah, huku mabasi mengine yakiachwa jambo lililotoa tasfiri kwa abiria hao kuwa pengine linatokana na mgongano wa kimaslahi baina ya watoa huduma hao, uongozi wa manispaa pamoja na wasimamizi wa huduma za usafiri.

Walipotafutwa kuthibitisha suala hilo, Uongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) umesema mgogoro uliopo na unaosababisha manyanyaso kwa abiria hayo unatokana na kiongozi Ofisa mmoja wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Temeke pamnoja na kiongozi kutoka Manispaa ya Temeke, na kwamba suala hilo wanalifuatilia.

“Inashangaza kuona kila siku ni kampuni hizi hizi mbili ndiyo zinayumbishwa pale katika eneo la kutoa huduma, kuna tatizo gani, nini kimejificha..kwa taarifa tulizozipata wapo watu wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi, jambo ambalo sisi kama uongozi wa wasafirishaji hatuwezi kulifumbia macho” amesema Katibu Mkuu wa TABOA Enea Mrutu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: