Spika wa Bunge (Mb), Mhe. Job Ndugai akizungumza wakati wa hafla ya uwasilishwaji na kukabidhi taarifa za Kamati Maalum alizounda  kuchunguza na kushauri kuhusu sekta za Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi asilia. Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma na mara baada ya kuzipokea taarifa hizo Mhe. Spika alizikabidhi Serikalini ambapo zilipokelewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa kwa niaba ya Waziri Mkuu.
 Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  kuchunguza na kushauri kuhusu Sekta za Gesi Asilia Mhe. Dustan Kitandula (Mb) akikabidhi taarifa ya Kamati hiyo kwa Mhe. Spika mara baada ya kuiwasilisha mbele ya Waheshimiwa Mawaziri, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa kitaifa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (kushoto) kwa Mhe. Spika
 Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  kuchunguza na kushauri kuhusu Uvuvi wa Bahari Kuu Mhe. Anastazia Wambura (Mb) akikabidhi taarifa ya Kamati hiyo kwa Mhe. Spika mara baada ya kuiwasilisha mbele ya Waheshimiwa Mawaziri, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa kitaifa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (kushoto) kwa Mhe. Spika
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akipokea taarifa za Kamati Maalum za Bunge kwa niaba ya Waziri Mkuu zilizoundwa kuchunguza na kushauri kuhusu Sekta za Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi Asilia kutoka kwa Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai. Wengine katika picha kutoka kushoto kwa Mhe. Spika ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na  Wajumbe wa Kamati Maalum ya Bunge aliyounda kuchunguza na kushauri kuhusu sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu (waliosimama) katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kutoka kushoto waliokaa ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Anastazia Wambura, Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi.  PICHA NA OFISI YA BUNGE.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: