Mume wa mtu anapotaka kulala na wewe au kutoka kimapenzi na wewe, atakwambia matatizo yote ya Ndoa yake, atamnasibisha mkewe kuwa ni mbaya na anatabia mbovu na atakuahidi kuwa atamuacha mkewe ili akuoe wewe.

Ataspend weekends na wewe, atakutambulisha kwa wanaume wenzake wenye tabia za umalaya kukuaminisha kuwa kweli anakupenda.

Lakini kabla hujafanya kosa kubwa katika maisha la kumkubali ngoja nikwambie kitu, wewe sio mwanamke wa kwanza kuambiwa na kufanyiwa hivyo na huyo mwanaume na wala hautakuwa wa mwisho.

Mke wake inawezekana anajua, na marafiki zake wanajua, hivyo basi yupo katika harakati za kukung'oa mtoto mzuri na ajisevie bila tatizo na sio kwamba ni kweli anakupenda.

Kamwe hatamuacha mkewe kwa ajili yako, hayo yalikuwa maneno tu ya kukulainisha ili uingie kingi. Hata kama kweli atamuacha mkewe basi hata wewe usubiri kusalitiwa vya kutosha na andaa kabisa moyo wa spear.

Go and get your life, najua maisha ni magumu hela hakuna. Na starehe pamoja na "SHOW OFF ZA INSTAGRAM" unazihitaji.

Ila hata kwa dakika tano tu kaa chini fikiria hayo maisha utaishi mpaka lini, na fikiria sana kuhusu mategemeo makubwa waliyo nayo wazazi wako juu ya wewe. Huwatendei haki.

Hapa mtaani ninapoishi kuna dada mzuri tu, kamaliza chuo mwaka jana hana ajira ila amejiajiri anatengeneza juice ya matunda, anawauzia majirani na nyingine huenda kuuza hostel za wanafunzi kila jioni.

Na maisha yanasonga vizuri tu. Analipa kodi ya chumba, anajivisha, na anakula kwa afya atakacho kwa jasho lake. Ukimuona huwezi fikiri kama ni muuza Juice. Hua namuita Malkia wa nguvu, wife material.

Sisemi wote muuze juice, la hasha ila tafuta mbinu ya kupata pesa kwa akili zako na si za kutegemea wanaume tena waume za watu.

Mnapaswa tu kufahamu kwamba mwanamke asie na akili, sehemu zake za siri ama hakika hupata shuruba sana.

Hayanihusu Anyway.

Rifat Abdallah ukweli Mchungu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: