Mkurugenzi mkuu mamlaka ya usafiri wa anga, Hamza Johari kulia pamoja na kaimu mkurugenzi wa udhibiti wa kiuchumi na biashara mamlaka ya usafiri wa anga Daniel Malanga kushoto mara baada ya zoezi la utiaji sani kumalizika leo Jijini Dar ea Salaam.
 Mkurugenzi mkuu mamlaka ya usafiri wa anga Hamza Johari akitia saini leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam ikiwa ni makubaliano ya kutekeleza mpango wa kuzuia magonjwa ya mlipuko yanayoweza kuambukiza kupitia viwanja vy ndege hapa nchini.
Picha ya pamoja wadau mbali mbali mara baada ya zoezi la utiji saini kunalizika leo katika ofisi zao jijini Dar es Salaam.

Na Agness Francis,Globu ya Jamii.

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) watia saini na wizara ya afya kutekeleza mpango wa kuzui magonjwa ya maambukizi kupitia viwanja vya ndege.

Mpango huo endelevu ulioanzishwa na shirika la ndege la kimataifa la usafiri wa anga duniani.

Ambapo kama wanachama wa shirika hilo ambao ni wadhibiti wa mamlaka ya afya nchini wanajukumu la kuchukua mpango huo na kuuandaa kwa kushirikiana na wizara ya afya pamoja na wadau mbalimbali wizara nyingine mbalimbali.

Akizungumza na vyombo vya habari leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam mkurugenzi mkuu mamlaka ya usafiri wa anga Hamza Johari amesema kuwa dhumuni ni kuhakikisha uboreshaji ili kujihakikishia Tanzania inapambana na magonjwa ya maambukizi yanayotokana na usafiri huo wa anga kwa njia ya muingiliano wa watu kutoka sehemu mbalimbali, ukizingatia nchi jirani ya jamuhuri kidemokrasia ya congo mlipuko wa ungojwa wa ebola umeshaua watu takribani 15.

Johari amesema pia ni utaratibu utakao wezesha utekelezaji wake ili kuhakikisha Umma wa usafiri huo wanasafiri kwa usalama.

Mkuu wa vituo vya afya wiwanja vya ndege,bandari na mipaka Remidius Kakulu amesema kuwa mpango huo ukianza utekelezaji wake itasaidia kupambana na maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama ebola ambapo chi ya kidemokrasia ya Congo ugonjwa huo umeshaua watu 15 kati ya 54 ambao ni wangonjwa.

"Katika viwanja vyetu vyote vya ndege tumefunga vipimo vya kupima joto ambapo abiria wote wanaoingia nchini watapimwa,kwa atakaeonekena na joto kali atawekwa pembeni kwa ajili ya uchunguzi zaidi"amesema Kakulu.

Aidha kaimu mkurugenzi wa udhibiti wa kiuchumi na biashara mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania Daniel Malanga amesema kuwa usafiri huo ambao wa haraka kuliko yote ndio unaoweza kusambaza magongwa kwa kasi zaidi kwa kutumia mpango huo muhimu kwa kushirikiana na wadau wengi wa viwanja vya ndege mbalimbali hapa nchin utasaidia kuzuia maambukizi hayo.

"Tukipewa taarifa kutoka wizara ya afya (WHO) kuwa kuna mgonjwa ambaye anavihatarishi vya maambukizo tunaweka mpango wetu tayari kwa kuanza kazi"amesema malanga.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: