SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI

Na Daniel Sarungi.

Katibu wa Wazalendo, Nasibugani.

Ndugu wazalendo Tunapoelekea katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani, embu tuchukue dakika chache kupitia yanayoendelea katika mgawanyo wa mipaka kwa Wilaya zetu , Mikoa na Majimbo.

Ni dhahiri kuwa katika uongozi huu wa awamu ya tano Rais wa JMT Mhe Dr John Pombe Magufuli amerejesha utawala bora na nidhamu katika kazi. Amesafisha sehemu mbali mbali ikiwemo vyeti feki, wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa n.k

Nakupongeza Sana Mhe Rais, nakuomba kama ukiona inafaa Usafi huu usiishie hapo, tufike na huku kwenye mgawanyo wa Wilaya zetu na majimbo.

Kwa kifupi tu Mhe Rais kuna Wilaya zina idadi ya watu chini ya elfu 50, na kuna Wilaya zina idadi ya watu zaidi ya milioni 1.

Lakini zote ni Wilaya na zinahudumiwa sawa kwa vyeo na nafasi za utawala kupitia kodi za Wananchi.

Mhe Rais na Wazalendo wote, Wilaya ya Kinondoni yenye takriban zaidi ya watu mil 1.7 ina majimbo mawili ya Uchaguzi, ukilinganisha na Mkoa mzima wa Pwani wenye watu chini ya mil 1.3 ina majimbo 9 ya Uchaguzi

Naomba pita na Mimi katika sehemu ya pili nikudadavulie kwa undani zaidi katika Wilaya zaidi ya 100 nilizotembelea nchi nzima.

#safishawilaya
#safishamajimbo
#twendepamoja
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: