Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mg'hwira akizungumza na waandishi wa habari katika kampeni maalumu ya kuzuia uharibifu wa miundombinu ya umeme mkoani humo.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi inayoendelea mjini Moshi.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro  Mhandisi Mahawa Mkaka akiwaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi ya umeme inayoendelea mjini Moshi pembeni ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Salama.
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro  Mhandisi Mahawa Mkaka akiwaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi ya umeme inayoendelea mjini Moshi pembeni ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Salama
Mafundi wa Tanesco wakikata miti iliyopita katika njia za umeme

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bi Anna Mg'hwira ametoa onyo kali kwa wakazi wa mkoa huo wanao jihusisha na uhabifu wa miundombinu ya Shirka la Umeme Tanzania (Tanesco) na kusema hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Mkuu huyo wa mkoa alisema, serikali inatumia gharama kubwa sana kuendesha shirika hilo hivyo kulihujumu kwa kuharibu miundimbinu sio sahihi na halivumiliki.

Aliyasema hayo jana wakati akiongea na waandisi wa habari, katika kampeni maalumu inayofanywa na Tanesco makao makuu ikiwa na lengo la kuhamasisha juu ya athari za kuhujumu miumbombinu ya shirika hilo.

“Hivi karibuni kumekuwepo na matukio ya baadhi ya watu kupoteza maisha baada ya kujaribu kujiunganishia umeme kwa njia ya wizi. naagiza wakazi wa mkoa huu kuacha kabisa tabia hiyo kwani matukio ya aina hiyo ni sawa na matukio ya uhujumu uchumi, ambayo yanarudisha nyuma jitihada za Serikali za kuhakikisha nishati ya umeme inapatikana na hivyo kufikia uchumi wa kati kupita viwanda,” alisema

Aliongeza kuwa uhujumu wa miundombinu sio tu inaleta hasara kwa shirika lakini pia inapelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa kupitia maafa mbalimbali ikiwemo vifo na ulemavu kwa watu wanaohusika na matukio hayo.

Naye Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kilimanjaro Mahawa Mkaka alisema changamoto ya uharibifiu wa miumbombinu unatokana na uelewa mdogo kuhusiana na madhara yatokanayo na umeme.

Pamoja na hayo shirika katika mkoa linajitahidi kufanya uhamasishaji wenye lengo la kuelemisha watu kujiepusha na uharibifu wa miundombinu.

“Tunatoa rai kwa wakazi wa mkoa huu kuwa madhalani wanataka kukata miti ambayo ipo karibu ya nyaya za Tanesco watoe taarifa ili wataalamu wetu wasaidie kwenye zoezi kwa kinyume na hapo wanaweza kupata matatizo ikiwemo kifo,” alisema meneja

Alisema kwa mwaka jana zaidi ya ajali zipatazo 30 ikiwepo ajali za moto na watu kupoteza maisha kutokana na matukio mbalimbali, “Nia ya shirika ni kuona tunamaliza mwaka bila ajali hata moja inayotokana na umeme,”

Aidha, maneja alisema kwa mwaka mkoa unapoteza asilimia mbili ya mapato yanayotokana na wizi wa umeme na uharibifu wa miundo mbinu ambapo fedha hizo zingetumika kuboresha zaidi upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Maneja huyo amewaomba wakazi wa mkoa huo kuendelea kushirikiana na shirika ili kuwabahini wanaoendeleza vitenda vya wizi na uharibifu.

Alisema mwaka jana pekee zaidi ya Sh50 milioni zilipatikana kutoka nafaini mbalimbali zinazotokana na uharibifu wa miundombinu.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: