Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimfariji mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe kufuatia kifo cha mama yake aliyezikwa leo wilayani Nzega. Kulia ni mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye na mbunge wa Kigoma Vijijini, Peter Selukamba. Wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Abdallah Bulembo wameshiriki msiba huo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa salamu za rambirambi katika msiba wa mama yake mzazi mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyezikwa leo wilayani Nzega.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (wa tatu kulia), Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamisi Kigwangalla (wa sita nyuma kutoka kulia), Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (wa nne kulia), viongozi wengine wa chama na Serikali na wananchi mbalimbali wakiwemo wa wilaya ya Nzega wakishiriki kusalia jeneza lenye mwili wa mama yake mzazi Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (haonekani pichani) muda mfupi kabla ya kupelekwa makaburini kwa ajili ya maziko wilayani Nzega leo.
Jeneza lenye mwili wa mama yake mzazi Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (haonekani pichani) likiondolewa kwenye eneo la makaburi kupisha mwili huo kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya milelel (kaburini) wilayani Nzega leo.
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (kulia), Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (mbele yake kulia) na viongozi wengine wa vyama na Serikali na wananchi mbalimbali wakiwemo wa Jimbo la Nzega wakishiriki kumzika mama yake mzazi, Hussein Bashe katika makaburi wilayani humo leo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: