Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Nandy Mwiyombella (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu makubaliano walioingia kati ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Kwese Infix kwa wateja wa Vodacom wataweza kushuhudia fainali hizo kwa kupakua App ya Kwese Inflix na kununua bando kupitia menu ya *149*01# na kuchagua vifurushi vya siku au wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Kwese TV Tanzania, Mgope Kiwanga na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Digitali Huduma za Ziada wa Vodacom, Paulina Shao. Picha na Cathbert Kajuna-Kajunason/MMG.
Mkurugenzi wa Kwese TV Tanzania, Mgope Kiwanga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kwese TV walivyijipanga kurusha michuano ya Kombe la Dunia kupitia App ya Kwese Inflix kwa wateja wa Vodacom Tanzania. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Nandy Mwiyombella.

Na Mwandishi wetu.

Mashabiki wa soka wanatarajia kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia inayoanza leo nchini Russia kupitia simu zao za mkononi kwa ushirikiano wa kampuni ya Vodacom Tanzania na Inflix.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Nandy Mwiyombella, alisema wateja wa Vodacom wataweza kushuhudia fainali hizo kwa kupakua App ya Kwese Inflix na kununua bando kupitia menu ya *149*01# na kuchagua vifurushi vya siku au wiki.

“Tunazindua kampeni yetu hii ya wateja wa Vodacom kushuhudia Kombe la Dunia tukiwa na Inflix, lengo letu ni kuwapa fursa wateja wetu kufurahia fainali hizi, tumeona tuungane kuwarahisishia wateja wetu kama ilivyo kauli mbiu yetu ya Yajayo yanafurahisha,” alisema.

Alisema kuwa kwa ushirikiano wa Vodacom na Inflix wamejipanga kuwaletea wateja wao kuangalia Kombe la Dunia kupitia Kwese Inflix bando kupitia simu ya kiganjani.

Naye Mkurugenzi wa Inflix, Mgope Kiwanga alisema kuwa wamejipanga kuleta mambo tofauti na sit u Fainali za Kombe la dunia bali kuna burudani za aina mbalimbali.

“Huu ni mwanzo tu wa kuwaletea mashabiki wetu kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia, tukiwa na Vodacom, mashabiki watashudia mechi zote katika fainali hizo pamoja na matukio na burudani mbalimbali,” alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: