Meneja wa DAWASCO wa Magomeni Mhandisi Damson Mponjoli akizungumza na waandishi wa habari wakati wa operesheni maalumu ya kufichua wezi wa maji iliyofanyika katika maeneo ya Magomeni Manzese, Manzese Midizini, Manzese Kilimahewa ampapo operesheni hiyo inaendelea maeneo mengine. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Moja ya maungio yaliyokuwa yakitumika kuiba maji na kuyaweka kwenye matanki kwa ajili ya kuyauza.
Mashine za kuvuta maji zilizokuwa zikitumika kuiba maji na kuyaweka kwenye matanki kwa ajili ya kuyauza.
Mtaa wa Magomeni Manzese zilipokamatwa mashine hizo.
Moja ya eneo zilipokuwa zimefungwa mashine.
Wananchi wakichota maji katika tanki la maji lililokuwa likijazwa na kuuziwa wananchi kwa shilingi 100/- kwa ndoo.
Wananhi wakitoa kero zao.
Maungo na tanki lililokuwa linajanzwa maji na kuuzia wananchi.
Meneja wa DAWASCO wa Magomeni Mhandisi Damson Mponjoli akitoa elimu kwa wananchi.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) imekamata mashine za maji (pump) zilizokuwa zimeunganishwa kwenye mabomba ya shirika hilo na kuwauzia wananchi kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa operesheni maalumu ya kufichua wezi wa maji Meneja wa DAWASCO wa Magomeni Mhandisi Damson Mponjoli amesema kuwa shirika halitaacha watu wanaohujumu shirika na kuathiri wananchi wengine wasipate maji.

Amesema kuwa licha waliojiunganishia maji kenyemela kukimbia lakini kidhibiti chao hakiwezi kukimbia hivyo hatua za kisheria zitafuata kwanza ni kujisarimisha kwenye mamlaka.

Mhandisi Mponjoli amewaomba wajumbe wa serikali za mtaa kupeleka orodha ya watu 50 ili kuwawekea vizimba vya maji ili kuondoa adha ya upatikanaji wa maji katika maoeneo yao.

Amesema kuwa miundombinu yote iliyokuwa imeunganishwa lazima ifumuliwe kutokana na watu hao kuunganisha mabomba hayo na kupitisha katika katika vyoo na mitaro ya maji machafu.

Mponjoli amesema kuwa yao walijiungia maji kiholela suala ambalo linahatarisha usalama wa afya za wananchi pamoja na shirika kukosa mapato ya kuendeshea huduma ya maji katika maeneo yao.

Katika operesheni hiyo wamekamata Mashine za Kuvuta Maji kutoka katika Mabomba makubwa ya dawasco, matanki Nane(8) ya Lita 10000,5000 na lita 2000.

Operesheni imefanyika katika maeneo ya Magomeni Manzese, Manzese Midizini, Manzese Kilimahewa ampapo operesheni hiyo inaendelea maeneo mengine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: