Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa, Muongoza Watalii wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe, Iddi Kaluse kuhusu Maporomoko ya Maji ya Kakombe ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.
Baadhi ya Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifuatilia Sokwe Mtu kwenye mapito yao ndani ya Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipanda mlima kwa ajili ya kuwaona Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.
Msafara wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ukielekea Hifadhi ya Taifa Gombe kwa kutumia usafiri wa boti.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye boti alipotembelea Hifadhi ya Taifa Gombe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma jana.
Mandari ya Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akicheza ngoma na kikundi cha Mwamgongo alipotembelea Hifadhi ya Taifa Gombe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akizindua rasmi kituo cha utafiti wa Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe ambacho kimefadhiliwa na Taasisi ya Jane Goodal, alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake mkoani Kigoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikata keki kama ishara ya kuzindua hafla fupi ya kuadhimisha miaka 50 toka kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake mkoani Kigoma. Anaeshudia kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu, TANAPA, Nyamakumbati Mafuru na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Donatus Bayona.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Gombe katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe alipotembelea hifadhi hiyo janawakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma jana.

Na Hamza Temba-Kigoma.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ameagiza wavamizi wote waliopo ndani ya Pori la Akiba Kigosi/Moyowosi na Hifadhi ya Msitu wa Makere mkoani Kigoma waondoke mara moja kupisha maeneo hayo yaendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na uongozi wa mkoa wa Kigoma, ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Alisema taarifa za kiitelijensia zinaonyesha kuwa wengi wa wavamizi hao ambao wameanzisha makazi, kilimo na ufugaji ni raia kutoka nchi jirani ambao pia wamekuwa wakijihusisha na uharibifu wa mazingira na vitendo vya ujangili.

"Haivumiliki kwa kiongozi yeyote mzalendo kwa nchi yake ambaye anajua kabisa maeneo yetu yamewekwa akiba kwa ajili ya uhifadhi na tunawazuia hata wananchi raia kuyatumia alafu wanakuja raia wa nchi nyingine wanaachiwa wafanye wanavyotaka, hapana hili halikubaliki" alisisitiza Dk. Kigwangalla huku akiutaka uongozi wa Mkoa huo usaidie kusimamia Sheria na wavamizi hao waondoke mara moja.

Aidha, ametoa kipindi cha miezi mitatu kwa watu wote waliovamia maeneo ya kinga za hifadhi (bafa) ambayo ni mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi na vijiji waondoke kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Katika hatua nyingine, Waziri Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Kigoma na Halmashauri husika pamoja na Wakala wa Huduma za Barabara TANROADS katika ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Mkoa huo na maeneo mengine.

Alisema, Serikali ya awamu ya tano imepanga kufungua Sakiti mpya za utalii ikiwemo ya Kanda ya Magharibi ambayo inaujumuisha mkoa wa Kigoma, hivyo ni lazima miundombinu ya barabara ijengwe na kuimarishwa ipitike muda wote ili hifadhi hizo zitumike zaidi kibiashara na ziweze kuchangia ipasavyo kwenye pato la Taifa kuliko ilivyo hivi sasa.

Ameuagiza pia uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu TFS kupima maeneo ya misitu ya vijiji jirani na Hifadhi ya Taifa ya Gombe ili kuona uwezekano wa kuyahifadhi kwa kutumia sheria za misitu na hivyo kutengeneza mapito muhimu ya Sokwe Mtu yatakayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Mahale na hifadhi za Misitu ya Tongwe East, Tongwe West, Masito East na Masito West.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Donatus Bayona alisema changamoto kubwa iliyopo katika hifadhi hiyo ni miundombinu ya barabara ya kuunganisha hifadhi hiyo na maeneo mengine ikiwemo mji wa Kigoma ambapo amesema kwa sasa hifadhi hiyo inafikika kiurahisi kwa kutumia usafiri wa boti.

Akiwa katika hifadhi hiyo, Waziri Kigwangalla alizindua tukio la kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa Hifadhi hiyo na kuzindua rasmi kituo cha utafiti wa Sokwe Mtu ambacho kimefadhiliwa na Taasisi ya Jane Goodal, pia alitembelea Maporomoko ya Maji ya Kakombe ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii ndani ya hifadhi hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: