Leo, Mahakama ya rufaa ya Tanzania, imetoa uamuzi dhidi ya Kampuni ya Yusuf Manji ya ughaibuni ya Golden Globe International Services Ltd na kampuni yake ya hapa nchini ya Quality Group Ltd, katika mgogoro juu ya madai ya Bw. Manji ya kupata hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya MIC Tanzania Limited, ambayo inatambulika kibiashara kama Tigo Tanzania. Madai makuu ya Bw. Manji yaliyotokana na amri ya siri ya Mahakama ya kuuza hisa kwa mnada pamoja na taratibu husika za utekelezaji.Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali madai hayo kwa sababu ya makosa makubwa yaliyofanyika. Millicom inayofuraha kuwa jaribio hili la kutwaa hisa zake limevunjwa na kwamba uamuzi wa Mahakama ya Rufaa umedhibitisha kuwa MIC Tanzania Limited (Tigo) inabaki kumilikiwa na kuwa chini ya mamlaka ya Millicom Group.


Naye msemaji wa Tigo Tanzania alisema: "Tumepokea na kuridhika na uamuzi huu wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Mahakama imesema kuwa jaribio la Golden Globe International Services Ltd la kutaka kujipatia hisa za MIC Tanzania Ltd  (Tigo) kwa mnada usio halali na bila taarifa yeyote kwa Millicom (Tanzania) NV limeshindikana. Tumejitahidi kupambana na makosa ya wazi na majaribio ya Bw. Manji ya kudhalilisha mfumo wa Mahakama ya Tanzania. Tunakubaliana na uamuzi wa Mahakama, amabayo inasisitiza mchakato wa ufuatiliaji wa sheria nchini Tanzania.

Tigo Tanzania ni kati ya watoa huduma wakubwa wa huduma za mawasiliano ya simu Tanzania na tunatarajia kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu wengi."
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: