Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya shamba la Misitu kutoka kwa Mkurugenzi wa Mipango-Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo kwenye uzinduzi wa shamba la misitu Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akikata utepe wakati wa kuzindua shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele mara baada ya kuzindua shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. (Picha na Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbuge wa Jimbo la Ileje Mhe. Janeth Mbene mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
Kikundi cha Ngoma cha Sange kikitumbuiza ngoma ya Ling'oma wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
---
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua shamba la miti katika hifadhi ya Misitu Iyondo Mswima lililopo Katengele wilayani Ileje mkoani Songwe ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.

Shamba hilo lililo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ni moja kati ya mashamba mapya yakiwemo Biharamulo (Chato Geita), Buhigwe (Kigoma) na Mpepo (Mbinga, Ruvuma).

Akisoma taarifa ya Shamba hilo kwa Makamu wa Rais, Mkurugenzi wa Mipango –Wakala wa Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo amesema kuwa mpaka shamba la miti la Iyondo Mswima limeweza kutoa ajira kwa wananchi 400 katika msimu wa kupanda miti, pia shamba limetoa ajira zingine 200 wakati huu wa maandalizi ya bustani ya miti, hekta 201 zimepandwa miti kama sehemu ya upanuzi wa mashamba ya miti ya Serikali ambapo bustani yenye jumla ya miche 430,000 kwa ajili ya upandaji miti wa mwaka 2018/2019.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele ambapo shamba la misitu la Serikali Iyondo Mswima limezinduliwa, Makamu wa Rais amewataka wananchi hao kutunza na kuyalinda mazingira kwa kupanda miti kwa wingi ambapo kila mwaka wananchi watapewa miche 50,000 na Wakala wa Huduma za Misitu wa Serikali.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: