Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii.

MTANDAO wa kijamii wa Facebook umekumbwa na poromoko kubwa la kihistoria katika soko la hisa baada ya kupoteza mapato kwa asilimia 19 na hii imeelezwa ni kutokana na watumiaji kupunguza kasi ya utumiaji wa mtandao huo.

Mmoja wa watafiti Thomson Reuters ameeleza kuwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 119 zimepotea kwa siku moja jambo ambalo ni historia katika soko la uchumi duniani.

Ameeleza kuwa mtandao huo hutumia mabilioni ya fedha katika kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama kwa watumiaji wake.

Poromoko hilo kwa mujibu wa jarida la Forbes limemshusha nafasi ya watu wenye utajiri zaidi duniani mmliki wa kampuni hiyo Mark Zuckerberg kutoka nafasi ya 4 hadi ya 6.

Hili si poromoko la kwanza kwa kampuni hii ya Facebook, ikumbukwe kuwa Julai 27, 2017 mapato yalishuka kwa asilimia 11.7 kwa siku.

Ikumbukwe kuwa mwezi Machi mwaka huu mtandao wa Facebook ulikumbwa na sakata la udukuzi wa taarifa za watumiaji zaidi ya milioni 50 ukihusisha uchaguzi nchini Kenya.

Mark Zuckerberg alianzisha mtanda wa Facebook (FB) mapema Februari 4, 2004 pia ni mtandao wenye watumiaji wengi zaidi duniani, mwaka 2010 Zuckerberg alitangazwa kuwa kijana mwenye ushawishi na tajiri kati ya matajiri 100 duniani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: