NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akizungumza na Mhandisi wa Maji Korogwe Mji Joseph Mcharo kabla ya kumsimamisha kazi kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akizungumza na watendaji wa Halmshauri ya Korogwe Mji wakati wa ziara yake.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa umakini Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe wakati wa ziara yake.

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amemsimamisha Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya Korogwe Mji Joseph Mcharo kwa kutumia force accout kwenye mradi wa zaidi ya Milioni 700 bila ya kibali toka Wizara hiyo.

Agizo la kusimamishwa kwa Mhandisi huyo alilitoa jana wakati akikagua mradi miwili ya maji ya Mtonga ambao umetumia zaidi ya milioni 700 na msambiazi ambao umetumia zaidi ya milioni 600 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya mkoa wa Tanga ambayo ilianza juzi wilayani Handeni.

Alisema mradi huo ulitakiwa kutumia kiasi cha shilingi Milioni 500 na wataalamu hao wakaubadilisha na kuufanya uwe wa milioni 700 ingawa bado unaendelea kusuasua jambo ambalo linaonyesha ubadhirifu wa fedha za Serikali

Akiwa kwenye mradi wa Mtonga baada ya kumalizika kuukagua alitilia mashaka na ndipo alipoamuru mhandisi huyo kumpatia maelezo ya kina kuhusiana na mradi huo lakini pia hakuridhika na maelezo hayo na kuagiza kuwa atapeleka wataalamu kutoka wizara ili kuweza kuhakiki thamani ya fedha na ubora mrai huo.

“Kwa kweli mimi hapa sijaridhika na utekelezaji wa mradi huu unaonekana upo chini ya kiwango na ucheleweshwaji huku wananchi wakiendelea kupata tabu hivyo nitatuma wataalamu kutoka wizarani waje kuhakiki mradi huo”Alisema

Baada ya ukaguzi wa mradi huo Naibu Waziri huyo aliambatana na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Korogwe mji kuelekea kwenye mradi wa Msambiazi ambako kunajengwa tenki kubwa la mradi utakaosambaza maji kwa wananchi.

Akiwa huku ndipo alipomuuliza mhandisi gharama za mradi ambapo alisema zaidi ya milioni 600 zimetumika kwa kutumia mfumo wa mkandarasi na kupelekea mradi huo kufikia kwenye hatua za mwisho jambo ambalo limeibua maswali mengi kwa Naibu Waziri na kuamua kuchukua uamuzi huo.

“Ndugu zangu haiwezekani mradi wa zaidi ya milioni 700 kutumia force account kinyume na taratibu za wizara huku mradi wa milioni 600 ukitekelezwa kupitia mkandarasi ni wazi kwamba kuna ubadhirifu unaendelea hapa na mimi sitakubali”Alisema.

Baada ya maelezo hayo Naibu Waziri aliamua kumsimamisha mkandarasi huyo kwa kigezo miradi inayotumia chini ya milioni 200 ndio inapaswa kutumia force acounti tofauti na alivyofanya mhandisi huyo huku akimdanganya kwamba anakibali kutoka wizarani.

Awali akijib u hoja za Naibu Waziri huyo Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Korogwe Mji Joseph Mcharo alidai anakibali cha wizara kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa mtonga kutumia force acounti ndipo Naibu Waziri huyo alipoamua kupiga simu wizara kupata ufafanuzi.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Halamshauri ya Korogwe Mji Jumanne Shauri alionekana kushindwa kujibu maswali ya Naibu Waziri jambo ambalo liliibuka mabishoni baina yao kabla ya Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe kumtaka Mkurugenzi akiri mapungufu yaliyojitokeza kwenye mradi huo.

Mradi wa Mtonga ambao Naibu Waziri Aweso aliitulia mashaka ni wa kusambaza tenki,mabomba na sehemu maalumu kwa ajili ya mtambo wa kutibia na kusafisha maji eneo la mradi husika
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: