Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akipokea cover ya tairi la gari lenye nembo ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia Myonga .
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiangalia uoto wa asili ambao hupatikana katika Hifadhi ya Taifa ya ya Ziwa Manyara wakati wa ziara ya kutembelea hifadhi hiyo hapo jana Jijini Arusha chini ya uratibu wa Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE).
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiwashukuru wasanii na wajasiriamali kutoka Jiji la Arusha ambao aliambatana nao katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani, iliyoratibiwa na Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE) lengo ikiwa ni kuwajengea watanzania utamaduni wa kupenda kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kukuza uchumi wa nchi.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa kwanza kulia) akingalia ramani inayonyesha vivutio mbalimbali pamoja na wanyama wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara jana Jijini Arusha wakati wa ziara ya kutembele hifadhi hiyo, wengine ni Rais wa taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE) Dkt. Godwin Maimu (katikati) na kulia ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia Myonga.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia Myonga kuhusu chemchem ya maji moto ambayo inapatikana katika hifadhi hiyo alipofanya ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wasanii na watanzania kwa ujumla lengo ni kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio hivyo.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Utalii Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara Bibi. Eva Mallya (kulia) baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) ikiwa ni hatua ya kuhamasisha utalii wa ndani chini ya uratibu wa taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE) Jijini Arusha. ( Picha na Lorietha Laurence-WHUSM, Arusha).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: