Walaka wa kampuni ya QNET wkitoa msaada wenye thamani ya zaidi ya milioni 9 kwa kituo cha watoto yatima cha Maunga mapema mwaka huu jijini Dar es salaam.
Walaka wa kampuni ya QNET wkitoa msaada wenye thamani ya zaidi ya milioni 9 kwa kituo cha watoto yatima cha New life orphange centre mapema mwaka huu jijini Dar es salaam.

Na Mwandishi Wetu.

QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inaamini katika maendeleo ya mtu binafsi na jamii kupitia kutengeneza fursa na inasisitizia falsafa hii katika biashara zake na katika shughuli zake za uwajibikaji kwa jamii.

Falsafa hii inatangazwa vyema zaidi kupitia kitengo cha kampuni cha uwajibikaji kwa jamii, RYTHM Foundation. RYTHM inasimama kama kifupisho cha Raise Yourself To Help Mankind, na kinajikita katika kanuni kwamba mtu anahitaji kujiwezesha yeye mwenyewe kwanza ili aweze kusaidia wengine kunyanyuka.

Foundation hii imeandaliwa kwaajili ya kutoa elimu, kuhamasisha na kufanya kazi na wengine kutengeneza maisha mazuri ya baadae ya wale wenye uhitaji. Inagusa dhamiri ya jamii na inatoa ukumbusho wa umuhimu wa kuleta tofauti katika maeneo ya kazi, jamii au umma kwa ujumla.

Tanzania ilikuwa miongini mwa nchi 13 za kiafrika ambako QNET iliungana na IRs kuleta shangwe kwa jamii mbalimbali za watu wasio na uwezo, wakati wa sikukuu za hivi karibuni za mwezi mtukufu wa ramadhani.

Kwa mujibu wa QNET, nguvu ya RYTHM inaendesha kampuni, wafanyakazi wake na wawakilishi binafsi (IRs) kuwafikisha katika mafanikio makubwa - na kutoa sadaka, hasa kwa jamii za watu wasiojiweza. Nguvu hii inaonekana wazi kupitia shughuli nyingi za CSR ambazo QNET inaziendesha kugusa maisha ya watu wasiojiweza kupitia misaada ya hali na mali katika nchi zote ambako inaendesha shughuli zake.

Nchini Tanzania, miongoni mwa manufaa yatokanayo na shughuli za QNET ni vituo viwili vya kulelea watoto yatima jijini Dar es salaam, makao makuu ya kibiashara ya Tanzania. Maunga Children’s Centre na New Life Orphans’ Home vyote vilipokea msaada wa vyakula vyenye thamani ya Tsh 18 Milioni, michango ambayo ilikusanywa na uongozi wa nchi mbili kama ishara ya ukarimu na upendo kutoka QNET.

Akiwa anatoa maoni kuhusu misaada ya QNET kwa watu wenye uhitaji mapema mwaka huu, Biram Fall alisema: "Msaada huu unaendana na mafundisho ya msingi ya RYTHM ambayo wakati wote yamekuwa yanalenga katika kuongeza juhudi zaidi katika kujali wale ambao hawana uwezo kwa kuwapatia mazingira mazuri ya kuishi kwaajili yao, hasa watoto ambao ni alama ya kizazi chetu kijacho."
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: