Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya TPA kwa mwaka fedha 2016/2017 uliofanyika katika  ukumbi wa Dar es Salaam Stop Centre jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imesema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 imeweza kuingiza meli 2,983 na kuingiza mapato zaidi bilioni 828 ikilinganishwa na mwaka fedha 2015/2016 ambapo iliingiza mapato zaidi ya sh. bilioni 734 kwa meli 2870.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema kuwa mapato yameongezeka kutokana na uchapakazi wa masoko yanayofaywa na Rais Dkt. John Magufuli katika kuwaunganisha na nchi mbalimbali katika utoaji wa huduma ya bandari.

Amesema kuwa katika mwaka fedha 2016/2017 kumekuwa na mafanikio katika utoaji wa huduma kontena na shehena mbalimbali hali ambayo imefanya wafanyabiashara kutumia bandari ya Dar es Salaam.

Mhandisi Kakoko amesema kuwa katika kipindi 2014/2015 wafanyabiashara walipungua lakini wamerudi kwa kasi kubwa na kufanya kuongezeka kwa meli, kontena na pamoja na shehena.

Amesema kuwa matokeo mengine ya kupata mafanikio ni kutokana na kufanya kazi kwa weledi katika kutoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam ikiwemo kudhibiti wizi mbalimbali uliokuwa ukifanyika.

Amesema kuwa katika mikakati waliojiwekea ni kuhakikisha wanapunguza muda wa wa kukaa bandari ili kuwafanya wafanyabiashara kupata huduma kwa wakati kutokana na kuwepo kwa dirisha moja ya kutolea huduma za bandari.

“Tutahakikisha tunafanya kazi kwa bidii katika kuwafanya watanzania wenye bandari yao wanaona faida ya kuwa na bandari kutokana na mapato yanayopatikana katika kuona huduma wanazohitaji kwa serikali wanazipata”. amesema Kakoko.

Amesema kuwa Rais Dkt. John Magufuli amekuwa Afisa Masoko Mkuu wa Bandari ambapo kumefanya kuweza kupata mafanikio ya kuongeza wafanyabiashara katika kutumia bandari ya Dar es Salaam.

Hata hivyo amesema kuwa kwamekuwa na ofisi katika nchi za Afrika Mashariki na nchi zilizo Kusini ambapo ofisi hizo zimekuwa na ufanisi katika kuongeza wafanyabiashara kutumia bandari ya Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: