Mkurugenzi, Mambo ya Watumiaji na Viwanda (DCIA) wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Raynold Mfungahema (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi wakati wa hafla ya kukabidhiwa leseni ya Masafa ya Mawasiliano katika bendi ya 700MHz iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya Vodacom kuibuka mshindi katika mnada ulioendeshwa na TCRA. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa kwenye hafla ya kampuni hiyo kukabidhiwa leseni ya Masafa ya Mawasiliano katika bendi ya 700MHz iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya Vodacom kuibuka mshindi katika mnada ulioendeshwa na TCRA hivi karibuni. Hafla hiyo imefanyika Makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc Hisham Hendi, leseni ya Masafa ya 700MHz, iliyotolewa na Mamlaka hiyo kwa kampuni ya Vodacom baada ya kuibuka mshindi katika mnada ulioendeshwa na TCRA mwezi Juni mwaka huu. Hafla hiyo imefanyika jijiji Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria wa Vodacom Tanzania Plc, Olaf Momburi na Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti (Head of Regulatory Affairs) wa Kampuni hiyo Ngayama Matongo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Hisham Hendi, akiongea wakati wa hafla ya kukabidhiwa leseni ya masafa ya 700MHz, iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kampuni hiyo baada ya kuibuka mshindi katika Mnada uliondeshwa na TCRA mwezi Juni mwaka huu. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa ujenzi ,Uchukuzi, na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe akiupongeza uongozi wa Vodacom wakati wa hafla ya kukabidhiwa leseni ya masafa ya 700MHz, iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Vodacom ilibuka mshindi wa mnada wa masafa ya Mawasiliano uliofanywa na TCRA hivi Karibuni. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi, Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha Sheria Olaf Momburi na Mkuu wa kitengo cha Udhibiti (Head of Regulatory Affairs) wa Vodacom Tanzania Plc Ngayama Matongo.
Waziri wa ujenzi, Uchukuzi, na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe (kushoto)akimpongeza kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi wakati wa hafla ya kukabidhiwa Leseni ya Masafa ya 700MHz, na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyofanyika makao makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, Vodacom ilibuka mshindi wa mnada wa masafa ya Mawasiliano uliofanywa na TCRA hivi Karibuni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: