Mbunge wa Jimbo la Vunjo,James Mbatia akisalimiana na Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Dkt Martin Shao alipowasili katika kata ya Mshiri-Marangu kwa ajili ya uzinduzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo.(katikati) ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawira .
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin Shao na viongozi wengine wa Dini wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa shughuli ya uzinduzi wa Taasisi ya Maendeleo katika Jimbo la Vunjo.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin Shao akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Vunjo wakati a uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin Shao akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la Vunjo,uzinduzi uliofanyika katika kata ya Mshiri-Marangu.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika uzinduzi huo.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria mkutano wa uzinduzi uliofanyika katika kata ya Mshiri -Marangu .
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akizungumza jambo na viongozi wenzake wa Dini waliohudhuria mktano wa uzinduzi wa taasisi hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawira akizungumza wakati wa mkutano huo .
Mmoja wa Viongozi wa Dini ya Kiislamu Sheakh ,Abdalah Mwacha akizungumza wakati wamkutano wa uzinduzi wa taasisi ya Maendeleo katika jimbo la Vunjo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba za viongozi zilizotolewa wakati wa Uzinduzi huo.
Diwani wa kata ya Mshiri,Exaud Mamuya akizungumza katika mkutano huo.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akikata utepe katika mtambo unaotumika kukarabati barabara ikiwa ni ishara ya kuanza kazi kwa Taasisi ya Maendeleo katika jimbo la Vunjo ambayo moja ya kazi zake ni kutengeneza barabara katika jimbo la Vunjo.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akibariki moja ya Mitambo itakayotumika katika kufanya matengenezo ya barabara katika jimbo la Vunjo.
Mtambo wa kukwangua barabara ukianza kazi muda mfupi baada ya kuzinduliw kwa Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo ambayo moja ya kazi zake ni kutengeneza miundo mbinu ya barabara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: