Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiongea mara baada ya kumaliza kufanya uzinduzi na ukaguzi wa mfumo wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid meter) . Pembeni ni Afisa Mtendaji Mkuu Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco). Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amepiga marufuku Mamlaka ya Bandari (TPA) kuacha kununua maji katika magari binafsi ya kusambaza maji kwa ajili ya matumizi ya kwenye meli na kuwataka wachukue maji kutoka mamlaka inayotambulika kisheria kufanya kazi hiyo.

Profesa Mbarawa ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa mita za malipo ya kabla(Pre Paid meter) au mita za Luku katika Hotel ya Sea Cliff, Kiwanda cha Pepsi, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) akiwa ameambatana na Uongozi wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco).

Akizungumza baada ya kutembelea TPA, Waziri Mbarawa amewataka mamlaka hiyo kuhakikisha maji yote yanayotumika katika meli zinazotia nanga bandarini yanatoka Dawasco.

Mbarawa amesema kuwa matumizi ya maji yanayotoka kwa wauzaji wa nje hayajulikani yanatoka wapi na usalama wake haujilikani kwahiyo yatakapokuja kuleta madhara kwa watumiaji ndani ya meli lawama zitakuja kwa serikali na sio wauzaji hao wa maji ya maboza.

“Napenda kuwaagiza Mamlaka ya Bandari kuachana na ununuzi wa maji kutoka mamlaka zisizohusika kwahiyo Kwahiyo masuala ya ujanja ujanja yaishe kuanzia sasa maji na na nakuagiza mtendaji wa Dawasco ukutane na Mkurugenzi wa bandari kwa ajili ya suala hili,” amesema Mbarawa.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa amechukua maagizo hayo kama aliyovyoelekezwa na Waziri.

Dawasco wamemfunga mita hizo na zitatumika kwa wateja wakubwa pamoja na viwanda ambapo mteja atahitajika kulipia maji kabla na kiasi ulicholipia kikisha basi maji yatakatika, mfumo huo utasaidia katika kuongezea mapato Mamlaka husika pia kwa watumiaji sugu waliokuwa wanadaiwa maji kwa muda mrefu watakuwa wanalipa madeni kila watakapokuwa wananunua maji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: