Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Bi. Beate Andrees anayeshughulikia masuala ya misingi ya haki mahali pa kazi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) alipomtembelea ofisini kwake Julai 24, 2018 Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wajumbe kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) walipomtembelea ofisini kwake kujadili miradi ya Shirika hilo ambayo wamekuwa wakitekeleza nchini. Julai 24, 2018 Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Wajumbe kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma. (Kulia Kwake ni) Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Eric Shitindi.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi akielezea jambo kwa wajumbe wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) (Hawapo Pichani) juu ya hatua ambazo zimekuwa zikichuliwa na ofisi yake kuhusu masuala ya kazi na ajira nchini. (Kulia Kwake ni) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.
 Bi. Beate Andrees kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) akimwelezea jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama. (Kulia Kwake) ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi pamoja na Wajumbe wengine kutoka ILO walipokutana Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani Afrika Mashariki Bw. Wellington Chibebe akimwelezea jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Wajumbe wengine kutoka Shirika hilo walipomtembelea ofisini kwake Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU - DODOMA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: