Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kulia) wakati akikagua mfumo wa namna mfumo wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid meter) kwa wateja wa majumbani.
Afisa Mtendaji Mkuu Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco), (kulia) akimwelezea Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa namna mfumo wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid meter) unavyo fanya kazi leo jijini Dar as Salaam. Picha na Cathbert Kajunason - Kajunason/MMG.
Moja ya mashine zilizofungwa kwa ajili ya wateja wa majumbani.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu toka kulia) akiwa na wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa DAWASCO.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kuzindua mfumo wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid meter).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akieleza machache wakati akikagua mfumo wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid meter).

Afisa Mtendaji Mkuu Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco), akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza uzinduzi wa mfumo wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid meter) unavyo fanya kazi leo jijini Dar as Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco), akikata utepe Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya SBC Tanzania Limited (PEPSI), Bw. Avinash Jha
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya SBC Tanzania Limited (PEPSI), Bw. Avinash Jha (wa tatu toka kulia) mara baada ya uzinduzi  wa mfumo wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid meter) kwa watumiaji wakubwa wa viwandani leo jijini Dar as Salaam.
Mashine zilizofungwa katika kiwanda cha kampuni ya SBC Tanzania Limited (PEPSI),  kwa ajili ya wateja wa majumbani.

Na Mwandishi Wetu.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Prof Makame Mbarawa ametoa miezi miwili kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaaam waliojiunganishia maji kinyemela kujisalimisha ofisi za Shirika la Maji safi na maji taka (Dawasco).

Hayo ameyasema leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufungaji wa mita mpya za malipo ya kabla (Pre Paid Meter) kwa wateja wakubwa na viwanda ambapo tayari wameshafunga katika Hotel ya Sea Cliff, Kiwanda cha Pepsi na Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Prof Mbarawa amesema wale wanaojiunganishia maji kinyume na sheria wajisalimishe kwa mamlaka zinazohusika na watakaobainika kujiunganishia maji kinyemelea watachukuliwa hatua za kisheria.

Amesema kuwa anafahamu wapo watu ambao wamejiunganishia maji na amewataja wajisalimishe wenyewe kwenye ofisi za Dawasco ili waweze kuingia katika mfumo unaofahamika na kupata maji kwa njia halali.

"Nafahamu awali kulikua na mlolongo wa jinsi ya kuunganishiwa maji ila kwa sasa wale wote waliojiunganishia maji kwa njia ya udanganyifu waende Dawasco ili waingia katika mfumo na zoezi hilo liwe ndani ya miezi miwili na kama hawatafanya hivyo wakibainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao," amesema Prof Mbarawa.

Kuhusu mita hizo za malipo ya kabla Mbarawa amesema zitasaidia kuleta nidhamu katika matumizi ya maji na kuliongezea mapato shirika na utasaidia katika kuondoa changamoto ya wizi wa maji pamoja na wadaiwa sugu ambapo watakuwa wanakatwa kila wanapoenda kununua maji.

Prof Mbarawa amewaagiza Dawasco kuhakikisha wateja wakubwa wote na viwanda wanawekewa mita hizo ndani ya mwezi mmoja na hilo lifanyika ndani ya wakati.

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema watatilia mkazo agizo la Waziri na wamejipanga kufanya kazi haraka inavyotakuwa na kuwafikia watumiaji wote ndani ya mwaka huu wa fedha.

Kuhusu upatikanaji wa vifaa, Mhandisi Luhemeja amesema wamejipanga na kuanzia sasa wateja wapya wataunganishwa kwenye mfumo huo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: