Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiangalia pikipiki zilizotolewa na wadau wa kupinga vita uhalifu kwa Kituo cha Polisi Muriet, kilichopo Kata ya Muriet. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi.Waziri Lugola yupo jijini Arusha kwa ziara ya kikazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola(wapili kushoto), alipotembelea nyumba za askari polisi zinazoonekana pichani, katika eneo la Kata ya Muriet,jijini Arusha.Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Ramadhani Ng’anzi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Kata ya Muriet, baada ya kutembelea Kituo cha Polisi na nyumba za askari polisi zilizopo eneo hilo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi (kushoto) kutembelea Kituo cha Polisi cha Muriet (kinachoonekana pichani) na nyumba za askari polisi zilizopo katika eneo hilo wakati wa ziara yake jijini Arusha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: