Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akitoa hotuba yake kwa wageni mbalimbali waliohudhulia dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumkaribisha rasmi nchini, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018. Kulia ni Mke wa Balozi Kazungu, Bi. Mapenzi Kazungu.
Kiongozi wa Mabalozi nchini na Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura akizungumza jambo kwa niaba ya Mabalozi wengine, wakati wakimkaribisha Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu, katika dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumkaribisha rasmi nchini, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018.
Kaimu Balozi wa Kenya nchini, Boniface Muhia akizungumza katika dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumkaribisha rasmi nchini Balozi mpya wa Kenya, Dan Kazungu, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018.
Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu (kushoto) akiwa katika mazungumzo yenye furaha na baadhi ya maafisa wa Ubalozi wa Kenya hapa nchini, wakati hafla fupi ya kumkaribisha Balozi huyo, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018.
Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akimkaribisha Kiongozi wa Mabalozi nchini na Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura wakati walipowasili kwenye hafla fupi ya kumkaribisha Balozi huyo, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018. Kulia ni Mke wa Balozi Kazungu, Bi. Mapenzi Kazungu.

Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akifurahia jambo na Kiongozi wa Mabalozi nchini na Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura. 
Balozi wa Namibia nchini Tanzania Mhe. Theresia Samaria akimkaribisha nchini Tanzania Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Kenya yaahidi kuendeleza undugu, Upendo na mshikamano baina ya nchi ya Tanzania.

Hayo yamesemwa na Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu wakati akizungumza kwenye sherehe ya ukaribisho iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Balozi Dan Kazungu amesema kuwa anamshukuru sana Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna kipekee kupokea hati yake ya utambulisho na kukubali afanye kazi nchini Tanzania, na ameahidi kuendeleza mshikamano na Upendo.

"Nipo hapa kuendeleza undugu, Upendo na Mshikamano baina ya nchi zetu ambao umejengwa kwa miaka mingi. Na nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nitashindwa kumshukuru Rais wangu Uhuru Kenyatta kwa kuweza kuniamini na kunipa wadhifa huu ili niwatumikie Wakenya na Watanzania.

"Binafsi Mimi si Mgeni Tanzania maana kipindi cha nyuma nilishawahi kuishi kwa muda wa miaka 7 nilikuwa meneja wa kampuni ya kimataifa ya IBM hivyo nimerudi nyumbani," amesema Balozi Kazungu.

Amesema kuwa amekuja nchini Tanzania kama kiungo muhimu ili kuweza kuhakikisha ndoto za Wakenya na Watanzania zinakamilika.

Nawashukuru Balozi 8 wa nchi za Afrika waliokuja kunipokea Mimi na familia yangu, hakika nimejiona mtu wa baraka, kwa vile sikutegemea jinsi nilivyopokelewa.

Kwa upande wake Balozi wa Rwanda nchini Tanzania amemuhakikishia mshikamano ili waweze kulisongesha gurudumu la maendeo la Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla linasonga mbele.

"Niwashukuru sana mabalozi mliojitokeza katika hafla hii ya kumkaribisha mwenzetu, nawaomba tuzidi kuendeleza upendo, Amani na mshikamano tulionao.

Katika hafla hiyo jumla ya mabalozi wapatao 10 waliweza kuhudhuria akiwemo Balozi wa Afrika Kusini, Namibia, Rwanda, Somalia, Misri na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: