MABADILIKO YA RATIBA:

Sagati sasa kuagwa Mnazi Mmoja saa 7 hadi saa 11

Mwili wa Marehemu Msemaji wa Wizara ya Viwanda, Shadrack Sagati sasa utaagwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam leo kuanzia saa 7 mchana hadi saa 11 jioni.

Mabadiliko hayo yanafuatia kubadilika kwa njia zilizotumika kuusafirishia mwili huo kutokea mkoani Geita hadi Jijini Dar es Salaam, hivyo kusababisha kusogeza mbele kwa ratiba hiyo.

Kwa maana hiyo mabasi ya kuwachukua waombolezaji nyumbani kwa marehemu Kitunda Polisi, sasa yataondoka saa sita mchana, badala ya saa mbili asubuhi kama ilivyotangazwa hapo awali.

Hata hivyo kamati ya maandalizi pamoja na wahusika wote mnaombwa kuanza kuwasili uwanjani Mnazi mmoja saa 5 asubuhi.

Imetolewa na:

Kamati ya Maandalizi
Msiba wa Shadrack Sagati.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: