Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu, akisalimiana na wananchi wa Kata ya Minyughemara baada ya kuwasili kwa ajili ya mkutano wa hadhara uliofanyika jana ambapo aliibua ubadhirifu wa fedha za mfuko wa jimbo hilo sh.milioni 1.6 unaodaiwa kufanywa na Mwenyeviti wa Kata hiyo, ambapo alitoa siku mbili awe amekamatwa.
Wananchi wa Kata ya Minyughe wakiwa kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Minyughe, Mheshimiwa Sadaki, akitoa taarifa ya maendeleo mbele ya mbunge.
Wananchi wa Kata ya Minyughe wakifuatilia mkutano huo.
Mbunge Elibariki Kingu, akihutubia katika mkutano huo.
Mbunge Elibariki Kingu, akimkabidhi kitita cha fedha mmoja wa wanakikundi cha uzalishaji katika kata hiyo.
Katibu wa Mbunge huyo, Abubakari Muna, akiwakabidhi fedha zilizotolewa na mbunge huyo, wasanii mbalimbali wa Kata hiyo.
Viongozi wa CCM wa Kata ya Minyughe, wakimkabidhi Mbunge wao zawadi ya kuku.
Mkutano ukiendelea.
Shukurani zikitolewa kwa mbunge na Mwenyekiti wa Kijiji cha Misake ndugu Chima.
Mbunge Kingu, akiserebuka na wananchi baada ya kuwahutubia wakati akielekea kupanda gari tayari kwa kuondoka.
Mbunge Kingu akipita juu ya makaravati wakati akikagua daraja linalo waunganisha wananchi wa Kata ya Mtunduru na Minyughe.

Na Dotto Mwaibale, Singida.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu, ametoa siku mbili kuhakikisha Mwenyekiti wa Kijiji cha Minyughe anakamatwa mara moja baada ya kudaiwa kufanya ubadhirifu wa sh.milioni 1.6 zilizo chuliwa kutoka katika akaunti ya mfuko wa jimbo hilo.

Kingu alitoa agizo hilo wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Minyughe iliyopo Wilaya ya Ikungi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana.

"Mwenyekiti huyu baada ya kupata taarifa kuwa nita kuja kufanya mkutano wa hadhara katika kata hii amekimbia akijua ni lazima nitaongelea kuhusu fedha hizo hivyo basi naviagiza vyombo vya dola kuhakikisha vinamkamata mara moja ndani ya siku mbili na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria kujibu mashitaka" alisema Kingu huku akishangiliwa na wananchi.

Katika mkutano huo Kingu aliweza kuzungumzia miradi inayofanyika katika jimbo hilo pamoja na kuchangia fedha zaidi ya shilingi milioni tatu kutoka kwenye mfuko wake binafsi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo pia alivikabidhi pesa vikundi vya ujasiriamali vilivyopo katika kata hiyo vinavyofanya vizuri.

Diwani wa Kata ya Minyughe Mheshimiwa, Sadaki katika mkutano huo aliweza kuelezea kwa umahiri matumizi ya fedha kutoka mfuko wa jimbo jinsi zilivyo tumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kufanyika.

Katika hatua nyingine uongozi wa kata hiyo ulimzawadia mbunge huyo uwanja wa kujenga nyumba yake ili aweze kuwa jirani kwa ajili ya kuwatumikia ambapo mbunge huyo ameahidi kuanza ujenzi mara moja.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: