Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (wa pili kushoto) akimpongeza mshindi wa gari la tano aina ya Renault Kwid la promosheni ya kusherehekea miaka kumi ya M-Pesa, Salum Chande Athumani wakati wa hafla ya kumkabidhi gari lake iliyofanyika katika Viwanja vya Zakhiem Mbagala jijini Dar es Salaam. Yamebakia magari matano ili kushinda mteja wa Vodacom unatakiwa kutumia huduma ya M-Pesa tu. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha maendeleo ya Biashara wa M-Pesa, Polycarp Ndekana na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Jacquiline Materu.
Mshindi wa gari la tano aina ya Renault Kwid katika promosheni ya kusherehekea miaka kumi ya M-Pesa,Salum Chande Athumani mkazi wa Mbagala Rangi Tatu akishuhudiwa na wazazi wake akipongezwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi wakati wa hafla ya kumkabidhi gari hilo iliyofanyika katika Viwanja vaya Zakhiem Mbagala jijini Dar es alaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (wanne kushoto) akiwa na wafanyakazi wenzake katika viwanja vya Zakhiem Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kumkabdhi mshindi wa gari la tano aina ya Renault Kwid la promosheni ya miaka kumi ya M-Pesa, Salum Chande Athumani ambaye ni mkazi wa Mbagala Rangi Tatu (hayupo pichani )
Wakazi wa maeneo ya Mbagala Kuu na viunga vyake wakiwa katika viwanja vya Zakhiem Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kumkabdhi mshindi wa gari la tano aina ya Renault Kwid la promosheni ya kusherehekea miaka kumi ya M-Pesa, Salum Chande Athumani ambaye ni mkazi wa Mbagala Rangi Tatu (hayupo pichani).
Mshindi wa gari la tano aina ya Renault Kwid la promosheni ya kusherehekea miaka kumi ya M-Pesa, Salum Chande Athumani mkazi wa Mbagala Rangi Tatu (katikati) akiwa na mama yake mzazi wakipagawishwa na msanii wa Singeli Msaga Sumu (wapili kulia) pamoja na kundi lake wakati wa hafla ya kumkabidhi gari lake iliyofanyika katika viwanja vya Zakhiem Mbagala jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: