Ni bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya The Mvula-Mandondo Band yenye makao yake nchini Uingereza,inayoongozwa na mwanamuziki mkongwe wa dansi mtanzania Saidi Jumanne Kanda aliyewahi kutamba na bendi za Super Matimila, na Bima Lee. 

Mkongwe huyo wa muziki anakiongoza kikosi chake cha Mvula-Mandondo Band katika jukwaa kubwa la maonyesho ya kimataifa ya GaiExpo trade fair yanayoambatana  International .Africa Festival Tübingen 2018 inchini Ujerumani ambalo mwaka huu "Focus country Tanzania". 

Bendi ya Mvula-Mandondo itapanda jukwaani kuanzia siku ya Ijumaa ya 10 Agosti 2018 hadi Jumamosi 11 Agosti 2018 Maonyesho hayo yanawashirikisha na Ujasilimali, wafanyibiashara, wasanii na wanamuziki na kuwakusanya umati watu zaidi ya laki moja katika viwanja vya Fest-Platz, mjini Tübingen, kusini mwa ujerumani.

Bendi ya Mvula-Mando inatarajia kutumbuiza katika onyesho lingine kubwa nchini Ufaransa mwezi Septemba.usikose kujumuika na waadau wengine katika maonyesho haya makubwa ambapo wasanii na wajasiliamali toka Tanzania wakiwakilisha na kupeperusha bendera ya "Hapa Kazi Tu"
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: