Mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Nane nane na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu,Benjamini Mkapa akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi wa Biashara wa Taasisi ya kusaidia sekta binafsi ya Kilimo nchini (PASS) Killo Lusewa baada ya taasisi hiyo kuibuka kinara wa maonesho hayo kwa taasisi zisizo za Kiserikali,maonesho yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Biashara wa taasisi ya kusaidia Sekta Binafsi katika Kilimo (PASS) akionesha cheti cha ushindi baada ya taasisi hiyo kushika nafasi ya kwanza kwa taasisi zisizo za kiserikali na kukabidhiwa na Rais Mstaafu,Benjamini Mkapa.
Wafanyakazi wa Taasisi ya kusaidia sekta Binafsi katika Kilimo(PASS) wakifurahia mara baada ya kutangazwa washindi wa kwanza kwa taasisi zisizo za Kiserikali katika maonesho ua nane nane ambayo yamefanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Wafanyakazi wa Taasisi ya kusaidia sekta Binafsi katika Kilimo(PASS) wakifurahia kwa pamoja na wanufaika wa msaada wa mikopo kutoka katika taasisi hiyo mara baada ya kutangazwa washindi wa kwanza kwa taasisi zisizo za Kiserikali katika maonesho ua nane nane ambayo yamefanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akikabidhi cheti kwa Meneja wa Taasisi ya kusaidia sekta Binafsi katika Kilimo (PASS) kanda ya Kaskazini ,Hadija Seif mara baada ya tasisi hiyo kutangazwa washindi wa pili kwa taasisi zisizo za Kiserikali katika maonesho ua nane nane ambayo yamefanyika mkoani Morogorogo .
Meneja wa Taasisi ya kusaidia sekta Binafsi katika Kilimo (PASS) kanda ya Kaskazini ,Hadija Seif akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa taasisi hiyo mara baada ya kutangazwa washindi wa pili kwa taasisi zisizo za Kiserikali katika maonesho ua nane nane ambayo yamefanyika mkoani Morogorogo.
Cheti kilichokabidhiwa kwa PASS,Morogoro.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa mkoani Simiyu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: