Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja akionesha moja ya mabango ya kutambulisha shindano la Jishindie Mamilioni.

Kutoka kushoto ni Phocas lusato Meneja Rasilimali watu SBC, akifuatia Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja na Hussein Mkwawa ambaye ni Meneja mauzo Kanda ya Ziwa wakisikiliza vyema maswali ya waandishi wa habari (hawako pichani) katika utambulisho rasmi wa shindano la Jishindie Mamilioni, uliofanyika ukumbi wa mikutano SBC Nyakato jijini Mwanza.
Nikama wakisemezana "Hebu tuone umepata nini ndani ya kizibo chako...." Balozi wa PEPSI Albert G. Sengo (kushoto) Sara Onesmo kutoka Clouds Tv na Johari Shani wa Mwananchi Communication.
Shindano hili la“Jishindie Mamilioni” litakuana vizibo vya rangi ya Silva. Shindano hili litakua na zawadi nyingi za pesa taslimu kuanzia shilingi za Kitanzania 1,000,000/-, 500,000/-, 10,000/-, 5000/-, 1000/= na SODA YA BURE.
Ili Mteja ajishindie zawadi anatakiwa kununua soda za Jamii ya Pepsi kisha abandue ganda Ndani ya Kizibo akikuta maandishi aidha ya shilingi 1,000,000/-, 500,000/-, 10,000/-, 5,000/- 1000/- au Free Pepsi (SODA YA BURE), atakua amejishindia zawadi hiyo papo hapo.

Zawadi za shilingi 10,000/=, 5000/=,1000/=na Soda ya bure zitapatikana hapo hapo kwa aliyekuuzia soda, Gari ya Mauzo au Muuzaji wa Jumla. Vizibo vya zawadi vimeandikwa kwa rangi ya dhahabu, Zawadi za shilingi 1,000,000/-, 500,000/- zitatolewa kiwandani Mwanza tu, Barabara ya Musoma, Nyakato, Kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 9 jioni siku za Jumatatu hadi Ijumaa (isipokua siku za sikukuu).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: