Mheshimiwa Musa Sima na Elibariki Kingu, wakiserebuka na wanachama wenzao wa CCM na wananchi huku wakiwa wamejitwika vibuyu. 'Hakika ina pendeza sanaaaaa.'
Mbunge wa Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu (kulia), ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Unyambwa Wilaya ya Singida mjini, Abdulazizi Hamisi Labu, akihutubia wananchi na wana CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Kitongoji cha Unyambwa Juu mkoani humo jana.
Mbunge wa Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu (kulia), akimdani mgombea huyo, Abdulazizi Labu.
Naibu wa Waziri wa Mazingira na Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mheshimiwa Musa Ramadhan Sima, akihutubia kwenye mkutano huo.
Kampeni Meneja wa uchaguzi huo, Selemani Hamisi Mdulu, akizungumza kwenye mkutano huo.
Wazee wa kata hiyo wakifuatilia mkutano huo.
Muonekano wa meza kuu kwenye mkutano huo.
Naibu wa Waziri wa Mazingira na Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mheshimiwa Musa Ramadhan Sima (katikati), Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Andrew.
Wanawake wa CCM wakiwa wamenyoosha mikono kumuombea kura mgombea huyo.
Mkuu wa Wilaya mstaafu wa Wilaya ya Nchemba, Francis Mtinga, akizungumza katika mkutano huo wakati akimuombea kura mgombea huyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Chifu ya Aledi Sylvester akizungumza kwenye mkutano huo.
Wabunge wakifurahi jambo kwenye mkutano huo. Kulia ni Mheshimiwa Aisharose Matembe na Mheshimiwa Elibariki Kingu.

Na Dotto Mwaibale, Singida.

MBUNGE wa Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu amewataka wananchi na wana CCM wa Kata ya Unyambwa Wilaya ya Singida mjini kumpa heshima Rais Dk.John Pombe

Magufuli kwa kumchagua mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulazizi Hamisi Labu.

Kingu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea huyo wa udiwani uliofanyika kitongoji cha Unyambwa Juu jana alisema hakuna heshima kubwa ya kumpatia Rais Magufuli zaidi ya kumchagua Labu kuwa diwani wa eneo hilo.

"Ndugu zangu wanananchi na wanaccm wenzangu hakuna heshima kubwa ya kumpa Rais wetu Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chetu Taifa kama si kumchagua Labu awe diwani wa kata hii kwani Magufuli ameonesha kutujali sana wananchi wa Singida" alisema Kingu huku akishangiliwa na wananchi ambao walisema watamchagua Labu.

Kingu alisema heshima kubwa ya kumpa Rais Dk.John Magufuli ni kuhakikisha wana mchagua Labu tena kwa kura zote ili aungane na Rais na mbunge wa jimbo hilo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na si kumchagua diwani kutoka chama kingine.

Alisema Rais Magufuli amekuwa na imani na wananchi wa Mkoa wa Singida kwani amekuwa akisaidia kupeleka miradi mikubwa kama ya maji na kuteua viongozi wa serikali hivyo hawana zawadi ya kumpa zaidi ya kumchagua Labu ili kuongeza kasi ya maendeleo katika kata hiyo.

Alisema Rais Magufuli anafanya kazi kubwa ya kuliletea taifa maendeleo kwanza ameanza kwa kuanzisha miradi mikubwa ikiwemo kununua ndege saba za kisasa mpaka wazungu wanamshangaa kwa utendaji wake, miji karibu yote sasa imewekwa taa, kubana matumizi kwani hapo zamani viongozi mbalimbali walikuwa wakipishana angani kwenda nje ya nchi ambapo walikuwa wakitumia fedha nyingi za umma lakini leo hii safari hizo hazipo tena na hata wao wabunge wanapata mshahara na posho za kuhudhuria bunge tu na si kama ilivyokuwa zamani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: