Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangalla akipokea CD ya albma ya Gold kutoka kwa msanii nyota wa Bongo flava Elias Barnaba 'Barnaba Classic' mapema leo Septemba 6, 2018, wakati alipotembelewa na msanii huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajali Agosti 4 mwaka huu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla akipokea CD ya albma ya Gold kutoka kwa msanii nyota wa Bongo flava Elias Barnaba 'Barnaba Classic' mapema leo Septemba 6, 2018, wakati alipotembelewa na msanii huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajali Agosti 4 mwaka huu. Kulia kwa Waziri ni Meneja wa Msanii huyo Michael Mlingwa 'Mxcater'
Na Andrew Chale, Dar.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla amempongeza msanii nyota wa kizazi kipya nchini Bongo flava Elias Barnaba maarufu kama kwa Barnaba Classic kwa hatua yake ya kutoa albam ya Gold ambayo itasaidia kukumtangaza zaidi kwenye medani za muziki ndani na nje ya nchi.

Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo mapema leo Septemba 6,2018 wakati alipotembelewa na msanii huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajali Agosti 4, na kumkabidhi rasmi CD ya album yake ya GOLD ambayo imeingia sokoni 31 August mwaka huu.

Katika hatua hiyo Waziri alimshukuru kwa kumtembelea ambapo pia alimpatia ushauri namna bora ya kuiuza albam hiyo ya GOLD ikiwemo soko la kimataifa.

"Nilipata mwaliko wako wa uzinduzi wa albam ya Gold. Bahati mbaya sikuweza kufika kutokana na ajari. Lakini naendelea vizuri na nashukuru kwa kufika kuja kuniona na kunikabidhi rasmi..natambua wasanii pia ni nguzo katika kukuza Utalii wetu ikiwemo kuutangaza kupitia ala na mashahiri yenu na ndio maana mwezi huu wa Septemba tunakuja na tamasha la Urithi ambalo Wasanii wamepewa nafasi ya kipekee" alieleza Waziri Dkt.Kigwangalla.

Kwa upande wake Barnaba alimshukuru Waziri Dkt Kigwangalla kwa kuipokea Album hiyo ambayo imezingatia vigezo vyote na ubora wa hali ya juu.

"Kwanza nikupe pole kwa ajali. Naamini wasanii na wadau wote tunakuombea upone haraka na urejee kwenye majukumu yako ya kila siku ya kukuza Maliasili zetu na Utalii kwa ujumla na upokee albam hii ya Gold ikuburudishe unapoendelea kuuguza majeraha, Asante Sana" alisema Msanii huyo wakati wa kumkabidhi Albam hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa Msanii huyo Michael Mlingwa Mxcater amesema albam hiyo iliyosheheni nyimbo Bora na kali zikiwemo Chausiku, Lover Boy na nyingine nyingi inapatikana katika maduka ya mtandao yaani (Online) kupitia Boomplay Music.

"Kwa watumiaji wa simu za smartphone wanaweza kuipakua kupitia App ya BoomplayMusic_tz na wataipata moja kwa moja" alisema Mxcater.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: